Habari za Mastaa

Keisha hajakata tamaa na siasa? Ray C na vurugu hospitali ya M’nyala, Young D na maana ya tattoo zake…255 (Audio)

on

CLLL

Kwenye zile stori zilizosikika kupitia 255 ya XXL, amesikika pia Keisha ambaye amezungumzia siasa na kusema zina changamoto kubwa sana ingawa anaipenda sana toka siku nyingi..anasema si kitu rahisi na hajakata tamaa licha ya kushindwa kwenye kura ya maon na kuahidi kujaribu tena.

keis

Keisha

Jana Ray C alichelewa kupewa dawa akiwa katika hospitali ya Mwananyamala Dar es salaam, kitendo hicho kilisababisha vurugu na kuvunjwa kwa kioo cha gari la muuguzi, mmoja wa wanaotumia dozi hiyo ambaye alishuhudia tukio hilo alisema Ray C baada ya kukosa dawa alianza vurugu huku akiwatukana wauguzi matusi huku akiwashawishi wenzake kufanya vurugu.

Inasemekana mpaka sasa bado yuko kituo cha Polisi Oysterbay.

raay

Ray C

Young Dee ni mmoja wa wasanii Tanzania wenye tattoo nyingi mwilini, leo kwenye Clouds Tv atachambua tattoo moja baada ya nyingine, amesema tattoo iliyopo kifuani imeandikwa kwa lugha ya Kihispania ikimaanisha ‘anashukuru’ yote aliyoyakuta duniani.

ypung

Young Dee

Wasikilize hapa wakizungumza kwenye 255 ya XXL.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Tupia Comments