Habari za Mastaa

Collabo ya Diamond na D’Banj? Vanessa kazungumzia tuzo za MTV, ‘Dear God’ ya Kala imevuka lengo?..(255 Audio)

on

onair

Diamond kambania collabo D’Banj? DBanj amesema aliwahi kukutana na Diamond na kutaka kufanya naye collabo lakini haikuwezekana.. sasa hivi wamepanga kufanya hivyo kabla ya mwaka kumalizika lakini hawajaweka wazi ni lini.

Diamond amesema walitakiwa kufanya wimbo wa pamoja lakini aliogopa kufanya kazi na msanii mkubwa kama huyo alafu ikatokea akashuka, inakuwa si kitu kizuri, alitaka kufanya kazi ngazi kwa ngazi ili kufika mbali.

dia

Diamond akiwa na D’Banj

Pamoja na kwamba Vanessa hakufanikiwa kurudi na tuzo ya MTV, Vanessa kikubwa anachojivunia ni kuweza kupata connections na wasanii wakubwa..amefanikiwa kurekodi wimbo na Patoranking, Sayi shay…pia wamerekodi wimbo wa miaka 10 ya muziki wa MTV akiwa na wasanii mbalimbali wakubwa.

VANEE

Vanessa Mdee aka Vee Money

Kala Jeremiah amesema mapokezi ya ngoma yake ya ‘Dear God’ umepokelewa na mashabiki wengi kuliko nyimbo zake nyingine..anaamini ulikua ni zaidi ya wimbo na anatarajia kufanya ngoma nyingine kali zaidi ya hiyo ili kutimiza malengo yake.

KALA

Kala Jeremiah

Wamesikika hapa wakihojiwa kwenye kipindi cha XXL CloudsFm…

Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments