Habari za Mastaa

Mr.Blue na Joh Makini wana bifu?, Bongo Fleva na Bongo Movie hawapendani? Pia Central Zone wamesikika..255 (Audio)

on

On Air sign in a studio broadcasting via radio, podcast or wireless transmission.

Kundi la Central Zone wameamua kuendelea na project ya kuchangia ujenzi wa maabara shule za Sekondari za Kata ambayo ilikuwa ni idea ya Betty Mkwasa…wamesema wamechagua maabara mbili zilizopo karibu nao ili kuhakikisha zinafikia lengo ili kuamsha mwamko kwa watendaji ili waweze kukamilisha zoezi hilo ambalo ni agizo la Rais Kikwete.

centa

Kundi la Central Zone kutoka Dodoma

Pia 255 imezungumza na Mzee Chilo ambaye amesema kwa sasa hawatumii Sound Track za wasanii wa hapa Bongo na wanazotumia kwa sasa ni za nje kutokana na za hapa kutaka mamilioni ya fedha..hakuna ushirikiano mzuri katika ya Bongo Fleva na Bongo Movie katika kushirikiana.

chiloo

Mr. Chilo wa Bongo Movie

Mr Blue pia kasikika kuhusu ngoma yake mpya ya ‘Kazi kwanza’ ambayo ametumia neno ‘mwamba’ katika wimbo wake hakumaanisha Joh Makini bali ni kutafuta vina…anasema anamuheshimu sana Joh Makini na hawezi kumkandia …anaamini jina la ‘Mwamba’ la Joh Makini pia amesema si jina lake halisi.

blll

Mr. Bue

Wasikilize hapa mtu wangu..

Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments