Habari za Mastaa

Barakah Da’ Prince baada ya ushindi wa KTMA, daftari la mashairi ya Linex.. Safari ya Fella na Yamoto South Africa.. #255 (Audio)

on

Enter

Leo kwenye 255 Barakah Da’ Prince amesikika akizungumzia kupata tuzo ya KTMA2015 na kusema imempa moyo sana wa kujiamini na kutambua nini anafanya.. kumbe alikuwa akihofia washiriki wote kwenye tuzo, na kama ngetokea hajapata tuzo hiyo yeye basi anaamini Alice kutoka THT angeweza kuibuka mshindi kama msanii Bora Chipukizi.

Said Fella amezungumzia safari ya Yamoto Band ambao leo asubuhi wameondoka kuelekea South Africa kufanya video ya wimbo wa ‘Cheza Kwa Madoido‘ ambapo kazi imekabidhiwa kwa Director Godfather.

Linex naye amesikika akizungumzia kupatikana kwa daftari lake lililopotea siku nyingi nyumbani kwao Kigoma ambalo ndani kulikua na mashairi yake ambayo alikua akiyahitaji sana katika kufanya kazi zake.. Kwenye daftari hilo kumbe Linex alikuwa kajaza mashairi tu na sio kitu kingine.

255 iko kwenye hii sauti hapa, play uwasikie wote na story zao zote.

Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments