Habari za Mastaa

At kashiriki kwenye wimbo wa Diamond? Said Fella na Bibi Cheka je?? Mona Gangstar na Young Killer…#255

on

255new

Ushirikiano ambao mara nyingi umekua ukitajwa wa wasanii wa Tanzania ni ule ambao kupitia kazi ya mwenzako unaweza kuifanya kama yako, At leo kwenye exclusive interview na 255 ya XXL amesema kuwa yeye ndiye aliyeshiriki kumtafuta mtu aliyepiga kinanda kwenye wimbo wa Diamond ule wa mduara wa Nasema nawe.

Headlines za kutokua sawa kiafya Bibi Cheka utakua umeshakutana nazo, Said Fella ambaye ni Mkurugenzi wa Mkubwa na Wanawe amesema kwa sasa Bibi Cheka anaendelea vizuri na muda wowote kabla ya mwaka 2015 kuisha utamsikia tena kwenye spika za radio yako mtu wangu.

Kutengana kwa kazi baina ya Young Killer pamoja na aliyekua Meneja na Producer wake Mona Gangstar zilianza kutoka katikati ya mwaka 2014,siku chache zilizopita Young Killer aliongea na 255 na kusema ikitokea kuna wimbo anatakiwa kufanya na Mona atafanya nae lakini kama atakataa basi ataenda kwa mtu mwingine.

Sasa leo Mona Gangstar amesema kwamba yuko tayari kufanya kazi na Young Killer lakini kama atakua tayari kulipia gharama za studio,unaweza kusikiliza mtu wangu kwa kubonyeza play hapo chini.

Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye TwitterFacebook na Instagram kwa kubonyezahapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahaukusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video yaAyoTVikufikie

Tupia Comments