Habari za Mastaa

Sikiliza 255 ya Clouds FM kupitia XXL Jumanne Novemba 12, 2014.

on

Nameless-Wahu-Wedding

Kwenye 255 Staa wa Bongofleva Ney Wa Mitego amesema hatamani watoto wake waje kufanya muziki kutokana na changamoto zake ila ikitokea yoyote akaja kufanya muziki hana tatizo atampa ushirikiano.

Stori nyingine kutoka 254 Kenya, Nameless na mke wake Wahu wamezungumzia kukasirishwa na uvumi uliosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu wawili hao kupeana talaka, kwa kile kinachosemekana kuwa ni matokeo ya vipimo vya DNA kuonyesha kuwa yeye sio baba halali wa mtoto wake wa pili.

Kupitia ukurasa wa facebook Nameless na Wahu wameelezea kukasirishwa na uvumi huo na kuelezea kushtaki mmiliki wa Blog iliyoanzisha uvumi huo kama fundisho.

Sikiliza kupitia 87.9 Clouds Fm Moshi.

Bonyeza play kusikiliza.

Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook

Tupia Comments