Habari za Mastaa

Story za kwenye 255 leo Novemba 27 tayari nimekuwekea hapa

on

AKundi la Weusi wamesema wamedhamiria kujenga Maktaba mia moja, ambapo wameanzisha kampeni waliyoipa jina la ‘Mia Mia Mwanangu’ ambapo wamesema watakuwa wakichangisha pesa kiasi cha shilingi mia kwa kila mtu ili kuweza kufanikisha mpango huo Maktaba 100 katika vijiji mia moja, ambapo kila maktaba itakuwa na vitabu mia moja.

Msanii Ommy Dimpoz amesema tayari ile video ya ‘Tupogo Remix’ imekamilika na anatarajia kuaiachia video ya nyimbo hiyo siku ya kesho Novemba 28, safari hii kampa shavu Director Adam Juma kuiandaa video hiyo.

Ommy amesema albamu yake imekamilika na ataiachia kuiachia mwakani siku ya Valentine.

Diamond Platnumz tayari ametua Afrika Kusini na asubuhi ya leo alikuwa ndani ya Jumba la Big Brother, ambapo mbali na kwenda kwa ajili ya kushiriki tuzo za CHOAMVA kuna project nyingine ya ONE ambapo ataungana na mastaa wengine kutengeneza nyimbo.

Jarida la New Africa limewataja mastaa pamoja na viongozi kadhaa ambao wana ushawishi mkubwa Zaidi ambapo Tanzania imeng’arishwa na mwanamitindo Flaviana Matata, huku Kenya ikiwakilishwa na muigizaji Lupita Nyong’o.

Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook

Tupia Comments