Mix

Mastaa walio kwenye headlines story za #255 leo >>> Diamond, MB Dogg na Young Dee.. (Audio)

on

entertainment_0

Story ya kwanza anasikika MB Dogg, alihit na ngoma kali sana lakini kwa sasa ni kama hasikiki sana, anasema kama wadau wakiamua kuweka nguvu nyingi kwa wasanii kama wao basi bado wana nafasi ya kufanya vizuri kwenye muziki.

MB DOGG

MB Dogg

Swali jingine kwa MB Dogg ni kuhusu wimbo gani aliowahi kuufanya ambao hata yeye anaukubali zaidi? Jamaa kasema wimbo wake ni wimbo wa ‘Ina Maana‘.. wimbo huo unamkumbusha vitu vingi pia vya siku za nyuma.

BOB Junior alisema wana mpango wa kufanya collabo na Diamond Platnumz.. Diamond amesema walishaanza maandalizi ya kuufanya wimbo huo, beat ikikaa sawa watafanya wimbo huo ila mpaka sasa hawajajua wataimba wimbo gani.

3

BOB Junior na Diamond Platnumz

Young Dee na Young Killer waliachia wimbo ambao kiukweli kwa mtaani ni hit.. Video yake je?

YOUNG+KILLER+&+YOUNG+D

Young Killer na Young Dee.

Young Dee amesema kuna vitu vilifanya video yao ikakwama.. Walitegemea mauzo mazuri kwenye wimbo wao mtandaoni lakini mauzo hayakuwa poa kwa vile wapo waliodownload na kuzisambaza, kwa upande wa mauzo wao haikuwa imekaa vizuri kwa hiyo wakakubaliana kwamba kila mmoja aendele na project zake.

255 iko kwenye hii sauti hapa, utazisikia story zote ukiplay mtu wangu.

Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments