Habari za Mastaa

Tuzo nyingine TZ.. Vee Money sasa hivi kwenye Magazine Marekani.. Mwana FA na Lamar kuhusu January Makamba >> #255 (Audio)

on

255

Mwisho wa wiki iliyopita kulitolewa Tuzo kwa watu mbalimbali pale Chuo Kikuu Dar Es Salaam, leo kwenye #255 kasikika Dr. Ulimwengu ambae amesema walitumia muda mrefu zaidi ya mwaka mmoja kufanikisha kila kitu mpaka hatua ya mwisho ya kutoa Tuzo hizo.

vanessa

Vanessa Mdee

Vee Money ameingia kwenye headlines pia.. Vanessa alipost picha mtandaoni kushukuru kampuni ya Magazine toka Marekani ambayo walimtafuta na kufanya nae kazi, tukae tayari kumuona kwenye kurasa za Magazine hiyo online any time akiwa na mastaa wengine kama Erykah Badu.

Jana June 07 2015 kulikuwa na mkutano wa January Makamba akitangaza nia ya kugombea Urais.. Kati ya mastaa waliokuwepo ni Mwana FA na producer Lamar.

FA & JM

Mwana FA na January Makamba wakipiga selfie.

Mwana FA amesema huu ndio mkutano wa kwanza kuhudhuria kwa vile anavutiwa na Siasa ya January Makamba ambae anazungumzia zaidi kuhusu njia za kutatua matatizo na sio kuyaelezea matatizo.. Lamar nae kasema katika vitu alivyovipenda ni ishu ya kujenga reli ili kumaliza tatizo la foleni.

Lamar

Producer Lamar

Iko hapa sauti ya 255 na stori hizo zote mtu wangu.

Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments