Story ya kwanza kwenye headlines za 255 inahusu staa wa Bongo Movie Aunty Ezekiel ambaye amejifungua jana MAY 21 2015.. Aunty aliandika post kwenye ukurasa wake wa Instagra, akionesha kufurahia ujio wa mtoto wake wa kike ambaye amempa jina la Cookie.
Diamond Platnumz nae kuna kingine kipya kutoka kwake, Nay wa Mitego alisikika kwenye 255 ya jana kwamba kuna wasanii underground ambao anawasimamia ili nao watoke kwenye game ya muziki, Diamond nae ana mpango huo kumbe !!
Jamaa amesema nae anamsimamia msanii mmoja underground; “Najua matatizo na shida anazokutana nazo mtu akitaka kutoka.. najaribu kuona namna gani naweza kusaidia mtu nae akasogea“– Diamond Platnumz.
Rapper Stereo aliwahi kutoa ahadi kwamba ana mpango wa kuachia ngoma ambazo atazirudia nyimbo za zamani za mastaa mbalimbali Bongo, kimya kingi kuna chochote kinaendelea?
Stereo amesema kazi zake kitaaluma zinambana anashidwa kukamilisha ratiba ya studio kurekodi, lakini mpango uko palepale na tayari ameanza kufanya nyimbo hizo muda wowote zikiwa tayari zitatufikia.
Hizi zote ziko kwenye hii sauti hapa, nimeirekodi 255 ili kama ulikuwa mbali na radio zisikupite kabisa
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.