Story kubwa leo June 28, 2017 ambazo zimepewa uzito kwenye vyombo mbalimbali vya habari kama vile Televisheni, Radio na Magazeti ni pamoja na issue ya Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa kuhojiwa na DCI kwa saa 4.
Pia zipo story nyingine kuhusu siasa, uchumi, jamii na utamaduni ambazo zimepewa headlines kwenye mitandao ya kijamii miongoni mwao ni Mwalimu ya Sekondari aliyejiua akiacha ujumbe kwa wanaomdai waende kwa Mkurugenzi.
Zote hizo na nyinginezo ambazo hukuzisikia, kuziona wala kusizoma nimekukusanyia na kupitia millardayo.com zitakufikia kwa namna ile ile.
Wakulima wa Wilaya za Karagwe na Kyerwa mkoani Kagera wamewashauri wenzao kulima kilimo cha kisasa ili kuongeza thamani ya mazao. #Mwananchi
— millardayo (@millardayo) June 28, 2017
Wanawake Geita wamelalamikia uwepo wa mfumo dume, elimu duni na imani potofu ktk jamii unaowazuia kuingia kwenye ujasiriamali. #Mwananchi.
— millardayo (@millardayo) June 28, 2017
Baada ya mapumziko ya Sikukuu ya Eid el Fitr, Bunge linatarajia kuendelea na vikao leo na kesho kabla ya kuahirishwa Ijumaa. #Mwananchi.
— millardayo (@millardayo) June 28, 2017
Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda ameitaka Serikali kuunda kikosi kitakachosaidia kumaliza mauaji Pwani. #Mwananchi.
— millardayo (@millardayo) June 28, 2017
Taasisi ya Uchungaji ya Tanzania Pastors Saccos Ltd ya DSM inatuhumiwa kuwatapeli wananchi zaidi ya 50 mkoani Arusha Tsh. 120m. #Mtanzania.
— millardayo (@millardayo) June 28, 2017
Uongozi wa Kaunti ya Kajiado, Kenya umewaamuru Watanzania zaidi ya 500 wanaoishi kwenye mpaka wa Namanga kuondoka ktk eneo hilo. #Mtanzania.
— millardayo (@millardayo) June 28, 2017
"Mmetoa mchango mkubwa mlipokuwa PDB nategemea mtaendelea hivyo katika ofisi mlizopangiwa." – Rais Magufuli. #Mtanzania.
— millardayo (@millardayo) June 28, 2017
Baadhi ya mafundi uashi na wauza vifaa vya ujenzi wamelalamikiwa kwa utapeli wakiuza bidhaa bila kuzingatia vipimo vya urefu/ujazo. #NIPASHE
— millardayo (@millardayo) June 28, 2017
Watanzania wametakiwa kujitolea kusaidia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu ili waishi vizuri kama watoto wengine. #NIPASHE.
— millardayo (@millardayo) June 28, 2017
Bunge litaunda Kamati kuchunguza Almasi ikiwa ni siku chache baada ya kuunda Kamati kuchunguza uchimbaji na biashara ya Tanzanite. #NIPASHE.
— millardayo (@millardayo) June 28, 2017
Jamii imetakiwa kuzitumia simu za mkononi kulisaidia Jeshi la Polisi kubainisha watu wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) June 28, 2017
CUF wanaomuunga mkono Maalim Seif wamesema hawaitambui taarifa ya kusajiliwa kwa Bodi ya Wadhamini wa Prof. Lipumba. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) June 28, 2017
Mwalimu wa Sekondari Rukwa amejiua akiwa nyumba ya kulala wageni akiacha ujumbe kwa wanaomdai kuwa waende kwa Mkurugenzi. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) June 28, 2017
Watoto 3 ambao ni majeruhi wa ajali ya basi la wanafunzi wa Lucky Vicent waliopo Marekani kwa matibabu watarejea TZ August. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) June 28, 2017
Mbunge wa Viti Maalum Rita Kabati ametoa elimu ya ujasiriamali kwa vijana 400 wa Kanisa Katoliki wa Parokia 10 Iringa. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) June 28, 2017
Watanzania wameshauriwa kuwapuuza wanasiasa wenye tabia za popo ambao hugeuka hata kwenye mambo ya msingi. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) June 28, 2017
Raia 45 wa Ethiopia wamekamatwa wakiwa wamejificha mashambani Tanga wakidaiwa kumsubiri mtu aliyekuwa anawatorosha kwenda A. Kusini. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) June 28, 2017
Rais JPM anatarajia kuwa mgezi rasmi katika ufunguzi wa Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Kibiashara 'Sabasaba' yatakayoanza leo. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) June 28, 2017
Imeelezwa juhudi za Rais JPM kupambana na ufisadi, watumishi hewa na kulinda rasilimali TZ zitafikia uchumi wa kati ifikapo 2025. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) June 28, 2017
Askari wa Jeshi la Polisi Konstebo Oresphory Salingwa amefariki na wengine 2 kujeruhiwa kwenye ajali ya pikipiki Kilimanjaro. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) June 28, 2017
Waziri Mkuu wa zamani Lowassa amehojiwa kwa saa 4 na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kwa tuhuma za uchochezi. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) June 28, 2017
Imeelezwa kuwa Serikali itakamilisha mradi wa maji wa Ng'apa, Lindi uliogharimu Tsh. 29b ifikapo mwezi July mwaka huu. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) June 28, 2017
Watoto mapacha wa Askari wa Usalama Barabarani Bukoba wamekufa maji wakisherehekea Sikukuu ya Eid el Fitr kwenye Ziwa Victoria. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) June 28, 2017
Rais wa Z'bar Dkt Shein amewataka madereva wa vyombo vya moto kuwa makini pindi waendeshapo ili kuepuka ajali zinazoepukika. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) June 28, 2017
Rais JPM amekutana na wataalamu wa umeme na ujenzi wa miundombinu ya mabwawa ya maji ili kujadili mradi wa kuzalisha umeme. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) June 28, 2017
Lowassa ahojiwa Makao Makuu ya Polisi kwa saa nne!!!