Jumamosi ya July 15 2017 timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars kwa wachezaji wanaocheza Ligi za ndani ilicheza game yake ya kwanza ya kuwania kufuzu kucheza michuano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza Ligi za ndani CHAN 2018 dhidi ya timu ya taifa ya Rwanda katika uwanja wa CCM Kirumba.
Taifa Stars ambayo ilikuwa nyumbani na italazimika kusafiri hadi Kigali tarehe 23 July kucheza mchezo wa marudiano, imelazimishwa sare ya kufungana goli 1-1, licha ya kuwa na sapoti kubwa ya mashabiki Taifa Stars walianza kuruhusu goli dakika ya 17 Rwanda wakaanza kuongoza kwa goli la Dominique Nshuti.
Mchezo ulizidi kuwa mgumu na hali ya mpira ikiwa asilimia 50 kwa 50, Taifa Stars wakapata goli la kusawazisha dakika ya 34 kupitia kwa nahodha wa Taifa Stars Himid Mao aliyefunga kwa mkwaju wa penati baada ya Lucogoza Aimambe wa Rwanda kuushika mpira katika eneo la hatari.
Taifa Stars sasa atakuwa na mtihani mzito July 23 2017 mjini Kigali Rwanda, watatakiwa kufunga kuanzia goli 1-0 au atoe sare ya kuanzia magoli 2-2 ili afuzu hatua inayofuata, Taifa Stars sasa itaendelea kuwepo jijini Mwanza hadi July 19 kwa ajli ya maandalizi ya mchezo wa marudiano.
VIDEO: Ulinzi aliyoingia nao Wayne Rooney uwanja wa Taifa leo