Kuelekea uchaguzi Mkuu wa shirikisho la soka Tanzania TFF unaotegemewa kufanyika August 12 2017 mjini Dodoma, wagombea wa nafasi mbalimbali ikiwemo za Urais wameendelea na kampeni zao kabla ya uchaguzi mkuu.
Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars na club ya Dar es Salaam Young Africans Ally Mayay Tembele ni moja kati ya watu waliyojitokeza kugombea nafasi ya Urais wa TFF, Ally Mayay amejitokeza kugombea nafasi hiyo huku akiungwa mkono na wimbi la wachezaji wa zamani.
Zamoyoni Mogele, Adolph Rishard na Mwalusako ni miongoni mwa wachezaji wa zamani wanaomuunga mkono Ally Mayay ambaye amezindua kampeni zake leo na kutaja kilichomsukuma na kikubwa atakachoanza nacho ni kujenga vision au dira katika soka la Tanzania.
“Kitu cha pili kilichonisukuma kugombea Urais wa TFF ni wakati unajua kila kitu kina wakati wake na hilo halikwepeki, miaka ya 60 na miaka ya 70 ni tofauti, malengo ya miaka ya 60 na 70 ni tofauti, zamani watu walikuwa wanacheza mpira kujifurahisha sasa hivi ni ajira” >>> Ally Mayay
VIDEO: Ushindi wa Simba vs Rayon Sports, Simba Day 8 2017 Full Time 1-0