Baada ya club ya Kagera Sugar kuiwekea pingamizi club ya Azam FC katika usajili wa mchezaji wa Taifa Stars Mbaraka Yusuph ambaye msimu huu amesajiliwa na Azam FC kama mchezaji huru akitokea Kagera Sugar.
Leo Ijumaa ya August 18 2017 mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Azam FC Jafari Iddi Maganga ameweka wazi kuwa wamefikia muafaka na Kagera Sugar kuhusiana na pingamizi lao la Mbaraka kuichezea Azam FC waliloliweka TFF.
“Kama mtakumbuka hivi karibuni Azam FC ilikuwa inahitajika na Kagera Sugar kuhusiana na mchezaji Mbaraka Yusuph ni mchezaji ambaye tumemsajili msimu huu akitokea Kagera Sugar lakini taarifa tulipata kuwa kuna pingamizi”>>> Jafari Iddi
“Kama inavyofahamika wachezaji wakisajiliwa majina yanaenda TFF na kuangali je kuna mchezaji ambaye amechukuliwa na club nyingine bila kufuata utaratibu? kwa hiyo kulikuwa na pingamizi kutoka Kagera kuwa mchezaji ana mkataba wa miaka mitatu, jana Kagera walikuja tumeongea nao na kufikia makubaliano ya kumruhusu Mbaraka kuichezea Azam FC” >>> Jafari Iddi
VIDEO: Ushindi wa Simba vs Rayon Sports, Simba Day 8 2017 Full Time 1-0