Top Stories

Walichosema Watanzania walioshinda Bajaj kutoka SportPesa

on

Promosheni ya SHINDA NA SPORTPESA inaingia siku ya 12 ambapo tayari washindi 11 wameshapatikana na zoezi la kukabidhi bajaji hizo likiendelea, watanzania wa rika zote kutoka kila kona ya Tanzania wameendelea kushiriki kikamilifu na kujishindia zawadi zao kutoka kwenye promosheni hiyo ambayo itadumu kwa siku 100 tangu ilipozinduliwa rasmi Oktoba 25 mwaka huu.

Kwa wiki nzima sasa, SportPesa imekuwa ikiingia mtaa kwa mtaa kutoa bajaji hizo aina ya TVS KING huku washindi husika wakielezea furaha zao sambamba na matumizi ya bajaji hizo.

Kubashiri hakuishii hapa

Cassian Anthony, mwalimu wa Shule ya Msingi Ngwelo wilayani Lushoto-Tanga alikuwa ni mshindi wa bajaji ya pili na aliamua kufunga safari kutoka Lushoto kuja kukabishiwa bajaji yake jijini Dar katika maeneo ya Kimara ambapo baba yake mdogo anaishi.

“Mzigo huu utafanyia kazi hapa hapa Dar ndio maana nimetumia nauli kutoka Tanga nimekuja hapa japokuwa niliambiwa mzigo naletewa kule lakini nikasema niufuate huku huku.

“Kwa kifupi nitaitumia kufanya biashara na kile kidogo ninachopata najua sasa hivi kitaongezeka, kwahiyo utakapoona vitu kama vile ujue hii ni nguvu ya SportPesa.

Kubashiri na SportPesa hakuishii hapa, kwasababu TVS KING zipo 100 naweza nikapata hata tano ila mara nyingine nikija tena hapa basi ujue ni kwa ajili ya Jackpot ile zaidi ya Milioni 200

Nilikatisha darasa

SportPesa pia ilitinga mitaa ya Mbagala Kibulugwa kukabidhi bajaji kwa Hussein Iddi Balo ambaye alikuwa mshindi wa bajaji ya tano, ambaye naye alitoa lake la moyoni.

“Wakati napigiwa simu nilikuwa kwenye shughuli zangu za taaluma. Nilishtushwa sana hadi darasa lenyewe nikalisitisha

“Nimejisikia furaha sana baada ya kubashiri na SportPesa ambapo niliweka mechi za Real Madrid, Everton na Southampton lakini nikapiga ndege wawili kwa jiwe moja, nimekosa kule lakini nikafanikiwa kushinda Bajaji aina ya TVS KING

Niliona masihara

Naye Joseph Mallya kutoka Himo, Kilimanjaro alikuwa ni mshindi wa bajaji ya nne na hakuona haja ya kusubiri aletewe kule kule alipo, akaamua kufunga safari ili kuja kukabidhiwa mzigo wake hapa hapa.

“Nimekuja hapa SportPesa kufuatilia ile bajaji ya TVS KING ambayo niliambiwa nimeshinda kwasababu sikuamini kwahiyo nikaamua nije mwenyewe kufuatilia.

“Nawashauri watu waendelee kucheza na SportPesa, kwasababu mimi mwenyewe kwanza niliona masihara lakini sasa hivi ndio naamini kama ni kweli na inabidi sasa nifanye biashara ya kusafirisha abiria.

Naye Sudi Mkwara kutoka Gongolamboto anakuwa mshindi wa bajaji ya nane. Sudi ambaye ni askari polisi wa kituo cha Kurasini anaamua kukabidhi mzigo kwa mzee wake ambaye anajishughulisha na uuzaji wa Samaki wakati ambao yeye atakuwa safarini kikazi.

“Kwakweli sikuamini kama ningeweza kushinda TVS KING kutoka SportPesa kwasababu najua wanaoshiriki ni wengi sana na hivi vitu vinategemea bahati zaidi.

“Mimi nasafiri kesho (Jumamosi) kikazi kwahiyo Bajaji hii nitamuachia baba yangu hapa nyumbani ambaye atakuwa anaisimamia na kitakachopatikana basi kitatumika kwa ajili ya kusomesha wanangu ambao ni wajukuu zake.

Jinsi ya kushiriki promosheni

Ili kushiriki kwenye promosheni hii ya SHINDA TVS KING NA SPORTPESA, kwanza kabisa unatakiwa kujisajili kwa kutuma neno GAME kwenda 15888 (kama bado hujajisajili), weka pesa kwa namba ya biashara 150888 kisha piga *150*87# au tembelea www.sportpesa.co.tz kuweka utabiri wako mara nyingi.

Ukishaweka utabiri wako, utatumiwa ujumbe unaokutaka kutuma neno SHINDA kwenda 15888 ili kuingia kwenye droo. Kadri unavyocheza mara nyingi ndivyo unajiongezea nafasi ya kushinda kila siku.

Manara kabeba TV na kuja nayo kwa Waandishi leo kuonyesha Simba inavyoonewa (+video)

Soma na hizi

Tupia Comments