Mix

Askari 14 watanzania wameuwawa DRC Congo

on

Ijumaa ya December 8 2017 Tanzania imezipokea taarifa za wanajeshi 14 wa jeshi la wananchi Tanzania JWTZ kuuwawa na waasi nchini DRC Congo, wanajeshi wa Tanzania walikuwa DRC Congo kama sehemu ya kikosi cha kulinda amani cha umoja wa mataifa UN.

Waasi wa ADF Jana Alhamisi ya December 7 2017 walivamia kambi ya MONUSCO iliyopo katika mji wa Beni na kufanya shambulio lililopelekea vifo vya askari 14 wa jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ na wamewajeruhi askari wengine 44 na wawili hawajulikani walipo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Antonio Guterres amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kulaani vikali kitendo cha waasi wa msituni wa ADF kuwaua askari hao waliyokuwa DRC Congo kama sehemu ya kikosi cha kulinda amani cha UN.

EXCLUSIVE: Ni kweli Godbless Lema na Meya Boniface wamepigana?

Soma na hizi

Tupia Comments