Ad
Ad

Mix

Makanisa mangapi yamesajiliwa Kenya? maombi ya kusajili kwa siku je?

on

Screen Shot 2014-02-03 at 1.44.25 PMStandard media Group Kenya imeripoti kuhusu Uhuru wa kuabudu nchini Kenya na jinsi ilivyorahisi kwa yeyote kuanzisha kanisa.

Wanasema uhuru wa kuabudu umesababisha kuenea kwa madhehebu ya kidini nchini Kenya huku hali ikizidi kuwa mbaya zaidi kutokana na ukweli kwamba kuanzisha kanisa nchini humo ni rahisi kama kuanzisha kituo cha misaada.

Ukihitaji kuanzisha kanisa, kinachohitajika ni kujaza fomu, uwe na katiba na ada ya usajili ya shilingi elfu mbili za Kikenya ambazo ni zaidi ya elfu 35 za Tanzania.

Baada ya kuwasilisha fomu na ada ya usajili itakulazimu usubiri kwa miezi mitatu na baada ya hapo utaanza kazi ya kanisa lako.

Kwa mujibu wa msajili, sasa hivi nchini Kenya kuna makanisa zaidi ya 10,000 yaliyosajiliwa ambapo kwa upande mwingine, kila siku msajili anapata maombi zaidi ya 100 ya watu mbalimbali wakitaka kusajili makanisa yao.

Katika visa vya makanisa nchini Kenya kuna kimoja nakikumbuka ambacho kiliripotiwa na NTV kuhusu mchungaji mmoja kumlipa mwanamke aliekua anajiuza barabarani, yani alimlipa ili akatoe ushuhuda wa uongo kanisani….

Alichotaka pastor ni umaarufu kwamba anaweza kuombea watu wakapona, watu wakilipata hilo na sadaka zitaongezeka pia….. unaweza kukitazama kisa kizima hapa chini.

Tupia Comments