AyoTV

Simba imetangaza kumpeleka Haruna Niyonzima India

on

Uongozi wa club ya Simba SC ambayo inaongoza Ligi Kuu Tanzania bara leo kupitia kwa mkuu wake wa idara ya habari na mawasiliano Haji Manara wametoa taarifa kuhusiana na majeruhi ya wachezaji wao kwa sasa.

Simba kupitia kwa Haji Manara imetangaza kuwa beki wao Salum Mbonde na golikipa wao Said Nduda baada ya kuwa majeruhi kwa sasa wameanza mazoezi mepesi mepesi na tayari wapo kambini na timu.

Kwa upande wa Haruna Niyonzima wametangaza kuwa ndani ya siku mbili hizi watampeka India kwenda kufanyiwa upasuaji mdogo baada ya kugundulika kuwa ufa katika mfupa mdogo wa mguu, upasuaji wa Niyonzima utamuweka nje kwa wiki mbili hadi tatu.

VIDEO:Goli la Okwi lililoidhoofisha Azam FC vs Simba katika mbilio za Ubingwa VPL

Soma na hizi

Tupia Comments