Michezo

Mabingwa wa Afrika Mamelodi Sundowns wamelazimishwa sare tasa na Azam FC

on

Baada ya Simba na Yanga kukataa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Mabingwa Afrika Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini kwa kigezo cha kutotaka kucheza mechi ya kirafiki kati kati ya msimu, Azam FC wao walikubali na kuingia uwanjani February 1 2017 kucheza dhidi ya Mamelodi.

Azam FC ambao ni Mabingwa wa Kombe la Mapinduzi 2017, waliingia uwanjani kucheza mchezo huo wa kirafiki wakiwa wanamkosa nahodha wao John Bocco, Sure Boy na Kingue  waliyokuwa majeruhi pia, hata hivyo kuwa na majeruhi haukuifanya Azam FC kuwa dhaifu.

Mchezo wa  Mamelodi Sundowns dhidi ya Azam FC haukuwa mwepesi, kiasi kwamba kila timu haikuweza kuona nyavu za mwenzake na kushuhudia mchezo ukimalizika kwa sare tasa 0-0, baada ya mchezo huo Mamelod wanaondoka Tanzania kutokana na kupata dharura na hawatacheza dhidi ya African Lyon.

VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4

Soma na hizi

Tupia Comments