Michezo

Kama ulisikia Claudio Bravo kujiunga na Man City, FC Barcelona wametoa kauli

on

Kwa zaidi ya wiki moja sasa toka taarifa za golikipa wa FC Barcelona Claudio Bravo aingie kwenye headlines akihusishwa  kukaribia kujiunga na Man City ya England, taarifa ambazo hazikuwa zimekanushwa wala kuthibitishwa na FC Barcelona.

August 21 2016 taarifa kutoka 101greatgoals.com inaeleza kuwa FC Barcelona wamethibitisha kukaribia kumuuza golikipa wao chaguo la kwanza Claudio Bravo kwenda Man City, FC Barcelona ambao wameanza msimu mpya wa Laliga kwa ushindi wa goli 6-2 dhidi ya Real Betis wamekubali kufikia makubaliano na Man City.

Baada ya ushindi dhidi ya Real Betis mkurugenzi wa michezo wa FC Barcelona Robert Fernandez alithibitisha kuwa wapo karibu kumuuza Bravo “Tumekubaliana na Man City kuhusiana na  uhamisho wa Claudio Bravo, kabla ya kufungua milango ya kuondoka kwa golikipa huyo lazima tusajili kwanza ndio tumruhusu”

ALL GOALS &PENALTIES : Azam FC vs Yanga August 16 2016, Full Time 2-2 penalties 4-1 

Soma na hizi

Tupia Comments