Bado siku nane Tanzania tuingie katika headlines za soka tofauti kwa kupata ugeni wa club ya Everton ya Ligi Kuu ya England ikiwa na wachezaji wake wa kikosi cha kwanza ambao watacheza game ya kirafiki na Bingwa wa Sport Pesa Super Cup Gor Mahia kutoka Kenya.
Mchezo huo ambao utachezwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam July 13, kabla ya mchezo huo Good news ikufikie kutoka kwa CEO wa Everton Robert Elstone ni kuwa akiwa na wataalam wa masuala ya biashara wa Everton watatoa semina ya siku mbili July 12 na July 13 kabla ya mechi.
Elstone akiongozana na wataalam wa masuala ya biashara wa club hiyo watatoa mafunzo kuhusiana na umuhimu wa club kumiliki uwanja wake na kuwa na miundombinu ya kisasa itakayoiwezesha club kukuwa kiuchumi.
Wengine watakaofaidika na semina ya Everton ni pamoja na makocha wa soka, wachezaji wa timu za vijana pamoja na waandishi wa habari ambapo watapata mafunzo maalum kutoka kwa wataalam wa Everton, kuonesha kuwa Everton imejipanga na yenyewe kuimarisha uchumi wa club yao utajenga uwanja wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 60000. tofauti na Goods Park ambao kwa sasa unachukua mashabiki 4157.
VIDEO: All Goals Taifa Stars vs Lesotho June 10 2017, Full Time 1-1