Habari za Mastaa

Inawezekana 2 Chainz kapigwa marufuku kuingia clubs za Las Vegas bila yeye kujua?!

on

2 chainz3

Wiki chache zilizopita msanii wa hip hop kutoka Marekani 2Chainz aliweka headlines kubwa baada ya kuambiwa alipe fine ya dola milioni 5 kwa ugomvi aliouanzisha kwenye moja ya shows akiwa backstage.

Leo kuna headlines mpya zinazomzunguka msanii huyu, kwa jinsi inavyoonekana sasa hivi 2Chainz anashindwa kupata mtonyo wa kuingia clubs zozote zilizopo jijini Las Vegas.

2 chainz4

Akiwa bado anashindwa kuelewa sababu za yeye kutokuruhusiwa kuingia kwenye clubs za Las Vegas, watu wengi wamekuwa wakiongea na kusema labda sababu za yeye kutokupewa nafasi hiyo imesukumwa na ugomvi aliyohusika nao na kauli chafu aliomtolea mwanamke mmoja siku hiyo.

2 Chainz hajakaa kimya, aliamua kuliongela suala hili kupitia page yake ya Instagram ambako alipost ujumbe unaosema…

2 chainz 5

>>> “kila nikijaribu kutoka na kwenda club Las Vegas wanasema nimepigwa marufuku… sipewi sababu, na sijawahi kueleweshwa kwa sababu gani, wanasema “harusiwi kuingia”, na hii ni mara ya kwanza kwa mimi kuweka issue zangu kwa social media lakini nahitaji kupewa sababu. Sidaiwi na casino yoyote, wala nini… kwa ufupi SIELEWI NINI KINAENDELEA” <<< 2 Chainz. 

Nimekusogezea post hiyo ya Instagram hapa chini.

2-chainz-instagram-post

Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments