Michezo

Rekodi aliyoiweka Guardiola baada ya kushinda tuzo ya kocha bora wa mwezi

on

Ligi Kuu England leo wametangaza tuzo tatu za mwezi December kama ilivyokawaida yake ya kila mwezi kutangaza mshindi wa tuzo ya kocha bora wa mwezi, mchezaji bora wa mwezi na goli bora la mwezi.

EPL wamemtangaza kocha wa Man City Pep Guardiola kuwa ndio mshindi wa tuzo ya kocha bora wa mwezi December kwa Ligi Kuu England EPL, ushindi huo unamfanya Guardiola kuwa kocha wa kwanza katika historia ya EPL kuwahi kushinda tuzo hiyo mara nne mfululizo.

Harry Kane

Guardiola sasa anakuwa kashinda tuzo hiyo jumla ya mara tano akiwa kaiongoza Man City katika michezo 60, wakati Jose Mourinho ameshinda tuzo hiyo mara tatu akiziongoza timu za EPL katika michezo 272, Harry Kane wa Tottenham ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi na Defoe akishinda tuzo ya goli bora.

Alichokifanya Simon Msuva kwa Wakati Ujao Youth Academy

Soma na hizi

Tupia Comments