Wakati wapenda soka wengi hususani waliyokuwa wanafuatilia robo fainali za michuano ya AFCON 2017 nchini Gabon, robo fainali ya mwisho ya Misri dhidi ya Morocco iliyokuwa inazikutanisha timu kutoka Afrika ya Kaskazini ilikuwa inasubiriwa kwa hamu huku wengi wakitamani kujua rekodi inavunjwa au itaendelezwa.
Morocco waliingia uwanjani wakiwa na rekodi imara dhidi ya Misri iliyodumu kwa miaka 21, kabla ya mchezo huu wa robo fainali uliyomalizika kwa Misri kupata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Morocco kwa goli lililofungwa na Mahmoud Kahraba dakika ya 87, Misri walikuwa hawajawahi kuifunga Morocco goli hata moja toka October 6 1996 katika mchezo wa AFCON uliyomalizika kwa sare ya 1-1.
Kwa ujumla Misri na Morocco zimewahi kukutana mara 27 katika mashindano tofauti tofauti, Misri akiifunga Morocco mara 3, akipoteza mara 13 na sare mara 11, ushindi huo unamfanya kila mchezaji wa Misri kupokea bonansi ya dola 1250 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 2.7 kutoka chama cha soka cha Misri.
https://youtu.be/xD1NgxvQJyY
VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4