AyoTV

AyoTV yamtembelea Mzee Kikwete “nanenepa siku hizi, mlikua mnanifuja”

on

Inawezekana wewe ni moja kati ya watanzania ambao wanatamani kumsikia au kufahamu shughuli za Rais mstaafu wa awamu ya nne wa Jahmuri ya Muungano wa Tanzania Dr Jakaya Mrisho Kikwete anaendeleaje na anafanya nini kwa sasa.
Unataka kufahamu malengo na mipango yake ya sasa ya Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete, Rais mstaafu Dr Jakaya Mrisho Kikwete kwa sasa yupo kijijini kwao Msoga Chalinze akijishughulisha na ufugaji wa ng’ombe wa maziwa na kilimo, AyoTV imepata nafasi ya kumtembelea nyumbani na shambani kwake.
DR Kikwete kwa sasa ana ng’ombe zaidi ya 400 ambapo mpango wake ni kuwa na majike  500 ya ng’ombe wa maziwa kwa ajili ya kuwa na maziwa mengi, ambapo akifanikiwa kuwa na uhakika wa kupata maziwa zaidi ya lita 2000 kwa siku anawaza kuanza kutengeneza siagi, yoghurt na maziwa.
UNAWEZA KUTAZAMA HAPA VIDEO YENYEWE RAIS MSTAAFU AKIONGOZA AYO TV KUANGALIA MIRADI YAKE YA KILIMO NA UFUGAJI MSOGA CHALINZE.


VIDEO: Ushindi wa Simba vs Rayon Sports, Simba Day 8 2017 Full Time 1-0

Soma na hizi

Tupia Comments