Mix

Uliipata MSG ya sheria mpya DSM? Kabla ya kupewa chumba Guest mnapigwa picha? Meya kaongea

on

Ijumaa ya May 6 2016 kama ni mtumiaji wa mitandao ya kijamii hususani Whatsapp najua utakuwa ulipokea ujumbe ambao ulikuwa unaripotiwa kuwa umetoka kwa meya  wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita, ujumbe uliokuwa umeenea ulikuwa unahusisha kuwa meya wa Dar es Salaam Isaya Mwita ametangaza sheria mpya.

Meya Isaya Mwita ameongea na millardayo.com na kueleza kuwa ujumbe unaoenea kuwa ametangaza sheria mpya Dar es Salaam sio wa kweli na umetungwa na watu ambao wanapanga kumchafulia jina lake.

ADAS

Ujumbe wa uongo ambao ulisambazwa leo May 6 2016 na kudaiwa umetoka kwa meya wa Dar es Salaam

“Sio kweli kuwa kuna sehemu nimetoa statement ya namna hiyo ila huyo atakayekuwa ameandika atakuwa na lengo tofauti, kwa hiyo naomba wananchi wapuuze hiyo statement ambayo imekuwa ikisambaa, bahati mbaya sikuwahi kupata mtu akiuliza maoni yoyote kuhusiana na tukio hilo la Kimara ila kwa upande wangu sijatoa tamko lolote”

Kama utakuwa unakumbuka vizuri usiku wa May 1 2016 millardayo.com iliripoti habari za mwanamke kuuwawa na mtu anayeaminika kuwa ni mpenzi wake kwa kudaiwa kuwekewa sumu kwenye chakula na mwanaume kuondoka kwa kumuaga mlinzi kuwa anaenda kununua vocha.

Unaweza sikiliza hapa sauti ya meya wa jiji la Dar es Salaam

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

KAMA ULIIKOSA HII: TUKIO LA MWANAMKE KUUWAWA KWA KULISHWA KITU KINACHOSADIKIWA KUWA SUMU GUEST KIMARA DAR ES SALAAM

Soma na hizi

Tupia Comments