AyoTV

VIDEO: Katibu Mkuu Yanga kuhusu Ibrahim Ajib na Niyonzima

on

Kutoka Makao makuu ya Club ya Dar es Salaam Young Africans Jangwani tunae Katibu Mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwasa ambae amekubali kujibu maswali  kuhusiana na kinachoendelea katika soka la Bongo hususani club yake.

Kuna stori kuwa Yanga wamemsajili Ibrahim Ajib wa Simba kimya kimya kwa dau la Tsh Milioni 50 na wamempa na gari aina ya Brevis ukweli upo ukoje kuhusu Ajib na kuhusu stori za Simon Msuva kuwa amepata club nje ya nchi na Yanga wamegoma kumruhusu?
Na hizi stori tunazosikia kuwa wameshindwana na kiungo wao wa kimataifa wa Rwanda Haruna Niyonzima ili aongeze mkataba ni kweli, yaani wameshindwa kumpa dau analolitaka na kuna habari kuwa kajiunga na Simba.
“Siwezi kusema lolote kuhusu Ibrahim Ajib na mimi nasikia kama unavyosikia wewe naona kwenye mitandao lakini niseme kuwa kuwa sina taarifa yoyote, kuhusu Msuva amepata timu Egypty na Morocco lakini hatuwezi kumruhusu aende hadi tupate mualiko rasmi” >>>Mkwasa
VIDEO: Alichoamua Rais wa Simba baada ya kupokwa point 3 na TFF vs Kagera

Soma na hizi

Tupia Comments