Mkuu wa vipindi wa Clouds FM radio na mgombea wa nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji ya shirikisho la soka Tanzania TFF Shaffih Dauda leo Ijumaa ya July 28 ametangaza kujitoa katika nafasi ya kugombea ujumbe wa kamati ya utendaji ya TFF.
Shaffih Dauda akihojiwa katika kipindi cha Clouds360 ametangaza kujitoa katika uchaguzi huo kutokana na siasa za mpira wa Tanzania, Shaffih amefikia hatua hiyo baada ya kuona mbinu na siasa chafu zinazoendelea dhidi yake.
“Mimi ni mfanyakazi wa #CloudsMediaGroup, nilikwenda Mwanza kwa ajili ya kazi. Hapa #Clouds tumelelewa kufanya kazi kwa bidii kufikia malengo na sitaki mambo yangu binafsi ( kugombea uongozi TFF ) uharibu malengo ya #NdonoCup na taasisi kwa ujumla”
“Nimehangaika kutengeneza jina langu kwa miaka mingi, natangaza kujitoa rasmi katika uchaguzi mkuu wa TFF na nitaendelea kuchangia kwenye maendeleo ya soka nchi hii nikiwa sio kiongozi ”
KAMA ULIIKOSA AUDI YA SHAFFIH DAUDA AKIELEZEA KUHUSU KUKAMATWA NA TAKUKURU