Siku tatu baada ya Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea kuhudhuria katika kanisa la Ufufuo na Uzima la Askofu Gwajima kwa ajili ya maombi ya kumuombea Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu aliyepigwa risasi na watu wasiojulikana.
Spika ameagiza kamati mbili za Bunge ikiwemo ya ulinzi kumleta Bungeni Mbunge huyo Saed Kubenea kesho kwa njia yoyote ili ajibu kauli alizozitoa kanisani hapo kuhusu Spika kudanganya idadi za risasi alizofyatuliwa Mbunge Tundu Lissu.
Hata hivyo Spika Ndugai pia ameagiza Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kumuhoji Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe kuhusu kauli alizozitoa kwenye mitandao ya kijamii.
AyoTV MAGAZETI: Wabaya wa Lissu waanza kutajwa, Wabunge kupima VVU Bungeni