Habari za Mastaa

Uongozi kuhusu kifo cha Mbalamwezi “Mwili umeokotwa hauna nguo” (+video)

on

Taarifa ya masikitiko iliyoripotiwa usiku wa kuamkia leo ni pamoja na hii ya kifo cha msanii wa kundi la The MAFIK aitwae Mbalamwezi ambapo baadhi ya ndugu wamesema taarifa za awali ni kwamba Mwili wake ulikutwa maeneo ya Africana Dar es salaam ukiwa hauna nguo ikiwa ni saa kadhaa zimepita toka msanii huyo atokomee bila kujulikana alipo.

Sasa AyoTV na millardayo.com zimempata Fredy Feruzi ambaye ni mmoja wa viongozi kutoka kampuni ya utayarishaji wa video ya Kwetu Studio ambayo inawasimamia wasanii The MAFIK na amezungumza haya kuhusu kifo cha msanii Mbalamwezi.

Taarifa juu ya kifo cha msanii Mbalamwezi, Muhimbili kuutambua mwili

Soma na hizi

Tupia Comments