Staa wa soka wa zamani wa kimataifa wa club ya Arsenal ya England Kolo Toure amepewa shavu na taifa lake la Ivory Coast baada ya leo October 5 2017 kumtangaza kuwa kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Ivory Coast.
Kolo Toure kesho October 6 2017 katika game ya Ivory Coast dhidi ya Mali ya kuwania kufuzu kucheza michuano ya Kombe la Dunia, atakuwa katika benchi kama kocha msaidizi akimsaidia kocha Wilmots.
Toure ambaye katikati ya mwezi September kocha wake wa Celtic Brendan Rodgers alimchagua kuwa msaidizi wake, ameendelea kuaminika na kupata nafasi kubwa katika nchi yake.
Kolo Toure mwenye umri wa miaka 36 alianza soka lake katika club ya Asec-Mimosas ya kwao Ivory Coast na baadae akacheza vilabu vya Ulaya kama Arsenal, Man City na Liverpool.
Cristiano Ronaldo ameuza tuzo yake ya Ballon d’Or