Jumanne ya July 4 2017 ndio siku ambayo kamati ya utendaji ya shirikisho la soka Tanzania TFF ilikaa kikao chake cha dharura, ajenda Kuu ikiwa ni kujadili kamati ya uchaguzi wa shirikisho la soka Tanzania TFF ambapo siku mbili nyuma mwenyekiti wa kamati hiyo Revocatus Kuuli alisitisha mchakato wa uchaguzi.
Kikao cha TFF cha dharura kilichokuwa kimekaa leo katika makao makuu ya shirikisho hilo, kiliongozwa na Makamu wa Rais wa TFF Wallace Karia na Kaimu katibu Mkuu wa TFF Salum Madadi.
Kikao cha kamati ya utendaji wa TFF kilikaa na kuamua kufanya mabadiliko kwa kuwaondoa baada ya wajumbe wa kati zinazohusika na uchaguzi kwa kigezo kuwa waliingia kimakosa, kama utakuwa unakumbuka vizuri kamati hiyo imekaa baada ya mwenyekiti kusitisha mchakato wa uchaguzi Mkuu lakini tarehe ya uchaguzi ipo pale pale.
UNAWEZA KUANGALIA HAPA MABADILIKO YALIOFANYWA NA KAMATI YA UTENDAJI YA TFF
VIDEO: All Goals Taifa Stars vs Lesotho June 10 2017, Full Time 1-1