Mix

VIDEO: Mpango utakaomaliza uhaba wa sukari Tanzania

on

Taifa la Tanzania mwezi May 2016 lilikuwa katika headlines nyingi kuhusiana na kuadimika kwa sukari, kiasi kwamba Rais John Pombe Magufuli kutoa onyo kwa wafanyabiashara wanaoficha sukari ili izidi kupanda bei, wakati hayo yakiendelea leo October 6 kampuni ya Quality Group Limited (QGL) imetangaza mpango wa kuanza kutatua tatizo hilo.

QGL wametangaza mpango wa kutatua tatizo la sukari kwa kujenga viwanda viwili vya sukari Tanzania, ujenzi ambao utaanza December  2016 na kukamilika 2018, viwanda hivyo viwili vitajengwa Pemba Zanzibar na Mkundi Morogoro ujenzi ambao utagharimu Tsh bilioni 21 za kitanzania kwa kila kiwanda.

img_0303

Stavros Isaakidis mshauri wa ufundi wa mradi huo

Ujenzi wa viwanda hivyo utakapokamilika 2018 vitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 100,000 za sukari zitauzwa ndani na nje ya Tanzania, lakini mradi huo pia unatajwa kuwa utaweza kutoa ajira 5000 za moja kwa moja na zisizo za moja kwa vijana wa kitanzania na wakulima wa miwa Tanzania sambamba na kumaliza uhaba wa sukari Tanzania.

Quality Group Limited itashirikiana na taasisi za serikali kama wizara ya kilimo, bodi ya sukari Tanzania (SBT), kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC), hata hivyo  QGL itafanya uzalishaji wa ethanol na umeme pia utakaounganishwa katika grade ya taifa.

Soma na hizi

Tupia Comments