Michezo

Good NEWS!!! Mtanzania ametajwa katika kikosi bora cha February Ujerumani (+Audio)

on

Kutoka Ujerumani katika mji wa Heilbrom millardayo.com imempata mtanzania Emily Mgeta anayecheza soka la kulipwa katika klabu ya Freund Spiel Lauffen inayoshiriki Ligi daraja la tano nchini Ujerumani, Emily leo ametangazwa katika kikosi bora cha mwezi February.

Emily ambaye alianza kucheza soka Ujerumani mwaka 2015 ametangazwa katika kikosi bora cha mwezi February cha Ligi daraja la tano Ujerumani inayoshirikisha timu 16 lakini hii ni mara ya kwanza kwa Emily kutajwa  toka aanze kucheza soka Ujerumani, millardayo.com imempata katika exclusive.

“Ni kweli nimechaguliwa katika kikosi bora cha mwezi February na hii ni mara yangu ya kwanza kuchaguliwa toka nimekuja kucheza soka hapa Ujerumani 2015, japokuwa hii sio timu yangu ya kwanza kuichezea hapa Ujerumani”

VIDEO: ALL GOALS: Simba vs Yanga February 25 2017, Full Time 2-1

Soma na hizi

Tupia Comments