AyoTV

VIDEO: Wagombea 57 wamejitokeza kuwania uongozi TFF

on

Kuelekea uchaguzi Mkuu wa shirikisho la soka Tanzania TFF, leo June 19 2017 list ya wagombea wa nafasi mbalimbali za Urais na Ujumbe wa kamati ya Utendaji inazidi kuongezeka kwa watu mbali mbali kujitokeza kuchukua fomu.

List ya wagombea waliyojitokeza leo ni pamoja na mchezaji wa zamani wa Yanga Ally Mayai ambaye leo amejitokeza kuchukua fomu na kusindikizwa na wachezaji wenzake wa zamani ambao wanamuunga mkono akiwemo kocha wa zamani wa Mwadui FC Jamhuri Kiwelu.

Kufuatia ongezeko la kuchukua fomu kuongezeka kwa kiasi kikubwa, list ya wagombe wa Urais hadi kufikia saa 8 mchana leo June 19 walikuwa wagombea 9 huku wa kamati ya utendaji wakiwa 48.

LIST YA WAGOMBEA URAIS TFF

1- Jamal Malinzi

2- Iman Madega

3- Wallace Karia

4- Fredrick Masolwa

5- Fredrick Mwakalebela

6- Athuman Nyamlani

7- Ally Mayai

8- Shija Richard

9- John Kijumbe 

VIDEO: Alichoamua Rais wa Simba baada ya kupokwa point 3 na TFF vs Kagera

Soma na hizi

Tupia Comments