Mix

Burna Boy kaacha historia London, ujio wake Tanzania Nov 29 mwaka huu

on

Ni headlines za Msanii wa Nigeria ambae pia ni mshindi wa tuzo ya MTV EMA 2019, Burna Boy ambapo Jumapili iliyopita aliweka historia katika Arena iitwayo The SSE huko London.

Staa huyo alivunja rekodi nchini Uingereza baada ya kuijaza Arena iitwayo The SSE yenye uwezo wa kuingiza watu Elfu 12,500.

Staa huyo baada ya kumaliza show yake alikabidhiwa chati chenye jina lake kama heshima aliyoiweka katika ukumbi huo.

Staa huyo ametajwa tena katika vichwa vya habari kutokea Tanzania kwamba mwezi huu tarehe 29 anatarajiwa kutoa burudani ya nguvu katika ukumbi wa Nextdoor Arena Dar es Salaam.

Staa wa mwisho kutokea Nigeria aliewahi kutoa burudani ya nguvu katika ukumbi wa Nextdoor Arena ni Davido kama ulimiss itazame hapa

Hii video ikimuonesha Davido alivyompandisha Diamond kwenye jukwaa la Nextdoor Arena Dar es Salaam

 

 

 

 

Soma na hizi

Tupia Comments