Michezo

Usisahau kuwa Yanga wamecheza na Ruvu Shooting leo March 1 2017

on

Baada ya Dar es Salaam Young Africans kupoteza mchezo kwa goli 2-1 siku ya Jumamosi ya February 25 2017 dhidi ya watani zao wa jadi Simba, leo Jumatano ya March 1 2017 ilicheza mchezo wake wa kiporo dhidi ya Ruvu Shooting uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Yanga wakiwa wameingia kucheza mchezo huo wa kiporo ambapo Ruvu Shooting ndio alikuwa mwenyeji, walionekana kuingia na tahadhari kubwa licha ya kuwa walikuwa wakicheza na timu iliyokuwa nafasi ya 10 katika msimamo, ukilinganisha na wao waliyokuwa nafasi ya pili.

Katika game hiyo ambayo Yanga walilazimika kumaliza pungufu kutokana na mshambuliaji wao mzambia Obrey Chirwa kuoneshwa kadi nyekundu, wamefanikiwa kupata ushindi wa goli 2-0, magoli ya Yanga yakifungwa na Simon Msuva dakika ya 31 kwa mkwaju wa penati na Emmanuel Martin aliyeingia akitokea benchi.

Ushindi huo sasa unaifanya Yanga kuendelea kuwa na nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu kwa kufikisha jumla ya point 52 nyuma ya watani zao Simba wanaoongoza Ligi kwa kuwa na jumla ya point 54, Ruvu wao bado wapo nafasi ya 10 kwa kuwa na point 28 wakicheza mechi 24, Yanga sasa atacheza dhidi ya Mtibwa Sugar siku ya Jumapili katika uwanja wa Jamhuri Morogoro.

ALL GOAL: SIMBA VS YANGA FEBRUARY 25 2017, FULL TIME 2-1

Soma na hizi

Tupia Comments