Michezo

VIDEO: Mtangazaji wa Clouds TV baada ya kunyolewa nywele, aliahidi atafanya hivyo Arsenal ikitolewa

on

Moja kati ya watu waliyowashangaza mashabiki wengi wa soka wiki moja iliyopita ni huyu mtangazaji wa Clouds TV James Tupatupa ambaye pia ni shabiki wa Arsenal ya England, Tupatupa aliahidi kama Arsenal itatolewa na FC Bayern Munich atanyoa nywele zote kichwani.

Ahadi hiyo James Tupatupa aliitoa baada ya Arsenal kufungwa goli 5-1 katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 bora uliyochezwa katika uwanja wa Allianz Arena mjini Munich Ujerumani, hivyo mchezo wa marudiano Tupatupa alikuwa na imani Arsenal yake itaishangaza dunia.

Kwa bahati mbaya Arsenal imetolewa kwa kufungwa kipigo kama cha mwanzo cha goli 5-1 na kuondolewa kwa jumla ya kufungwa goli 10-2, Tupatupa

“Presha ya mchezo wa jana ilikuwa nzuri kwa pande zote mbili lakini mchezo uliamuliwa na refa baada ya Kolselny kuoneshwa kadi nyekundu, kwa hiki kitendo kimenikumbusha kuwa nisiunganishe utabiri na kitakachoenda kutokea uwanjani kitu kama soka ni ngumu kutabiri”

ALL GOALS: SIMBA VS MBEYA CITY MARCH 4 2017, FULL TIME 2-2

Soma na hizi

Tupia Comments