Burudani

BBC imetaja wanawake 100 wenye ushawishi 2017, Afrika wametajwa 8

on

Shirika la utangazaji la Unginereza maarufu kama BBC ni moja kati ya mashirika makubwa  ya habari duniani na yenye heshima kubwa kila kona ya dunia, licha ya BBC kuwa na utamaduni wa kutoa tuzo na kutambua michango ya watu mbalimbali kutoka tasnia tofauti tofauti.

BBC wametaja list ya wanawake 100 wenye ushawishi, BBC imetaja list hiyo na kwa upande wa bara la Afrika wametajwa wanawake nane na huku Afrika Mashariki wakitajwa wanawake watatu wanaotokea Kenya ambao ni Adelle Onyango, Anita NderuNaomi Mwaura.

Anita Nderu wa Radio na TV

Wanawake wengine wa Afrika waliyofanikiwa kupata heshima ya kutajwa na BBC katika list hiyo kutokea Afrika ni pamoja na muimbaji kutokea Nigeria Tiwa SavageChaima Lahsini wa MoroccoEllen Johnson Sir leaf wa LiberiaMarieme Jamme wa Senegal na Talent Jumo wa Zimbabwe.

Adelle Onyango ni mtangazaji wa Radio

Naomi Mwaura ni Founder, Flone Initiative and Communications Associate wa ITDP Afrika

Style aliyotumia Diamond Kumuwish Wema Sepetu kwenye birthday yake

Soma na hizi

Tupia Comments