Watu watatu wamefariki na wengine 32 wamelazwa hospitalini nchini Ufilipino baada ya kula kasa wa baharini.
Maafisa wanasema, makumi ya watu kutoka jamii ya Teduray waliripoti kuhara, kutapika na tumbo kuuma tangu kula kitoweo hicho wiki iliyopita katika mji wa pwani wa jimbo la Maguindanao del Norte.
Ingawa ni kinyume cha sheria kuwinda au kula kasa wa baharini chini ya sheria za ulinzi wa mazingira za Ufilipino, viumbe hao bado wanaliwa katika baadhi ya jamii.
Lakini kasa wa baharini ambao hula mwani mchafu, wanaweza kuwa na sumu wanapopikwa na kuliwa.
Mapema mwaka huu, watoto wanane na mtu mzima mmoja walikufa baada ya kula nyama ya kasa katika kisiwa cha Pemba katika visiwa vya Zanzibar, Metro iliripoti.
Watu wengine 78 walilazwa hospitalini baada ya kula chakula hicho Machi 5, kwa mujibu wa Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mkoani, Dk Haji Bakari.