Mbali na kwamba tuliona Diamond Platnumz na Majizzo kuingia headline za umiliki wa vituo vya Radio vya urushaji wa Matangazo nchini.
Sasa Meneja Sallam Sk nae hakusubiri mwaka huu uishe bali nae anamiliki kituo kipya cha Radio kiitwacho Mjini Fm ambacho Frequency zake ni 92.5 fm kama ukiwa Dar es Salaam ama Zanzibar utaisikia kwa umakini kabisa.
Kituo hicho kina miezi kadhaa tangu kianze kurusha matangazo yake na miongoni mwa watangazaji waliopewa dhamana ya kutangaza katika kituo hicho ni Jimmy Kabwe, Abby Plaatjes, Soggy Dogg, Binah Kasembo na wengineo.
Akizungumza na Millardayo.com Mkurugenzi wa kituo hicho Sallam Sk alisema..”Imekuwa ni ndoto yangu ya muda mrefu na ukimya wangu umetoa majibu kwamba hiki ndicho nilikuwa nakimpambania usiku na mchana si kitu rahisi sana lakini mpaka kufikia hapa nilipo ni hatua kubwa napenda kumshukuru Mungu sana”– Sallam SK
“Na nimeingia katika Challenge ambayo sio ndogo katika upambanaji bali ni kubwa sana unajua kumfanya mpaka msikilizaji asikilize Radio yako si kitu rahisi inategemea wewe umeandaa kitu gani kitakachomfanya asikilize kimvutie kwahiyo kuna vitu vingi vipya vinakuja wapenzi wa Radio watengee sikio 92.5 ndio Frequency yetu masafa yapo mpaka Zanzibar hata ukiwa Dsm unatupata’- Sallam SK
“Radio hii ni yetu sote nawakaribisha wadau, wanasiasa kufanya kazi na 92.5 Mjini fm ofisi zetu ziko mkabala na Shule ya IST Masaki Dar es Salaam ndipo ofisi zetu kwasasa zipo hapo za awali ukiuliza tu Mgahawa uitwao Hamu basi utakuwa umefika katika ofisi zetu”- Sallam Sk
“Pia napenda kuwashukuru watangulizi wangu wakina Kusaga, Majizzo na wengine najua tutashirikiana zaidi katika hili kuhakikisha kila mmoja anakuwa na mawazo chanya kwenye kufikisha kile kinachotakiwa katika jamii kupitia Radio zetu”– Sallam Sk