Habari za Mastaa

Kaka anasema Maria Carey kakataa kumlipia matibabu dada yake anayeishi na virusi vya UKIMWI

on

Kaka mkubwa wa Pop Queen Maria Carey, Morgan Carey (51) ametokea hadharani na kutoa lawama na ukweli kuhusu msimamo wa Maria Carey kukataa kutoa pesa ya kumtibu au kusaidia malipo ya matibabu ya dada yao ambaye anaishi na virusi vya UKIMWI.

Morgan amemlaumu Maria kwa kuonyesha kuwajali Mbwa wake na kuwalisha chakula kizuri zaidi wakati kakataa kulipia matibabu ya dada yao anaeonekana kukata tamaa ya maisha ikiwa hii sio mara ya kwanza kwa Maria Carey kuipotezea familia yake, kuna kipindi kaka huyu alifiwa na mtoto wake na Maria hakujibu taarifa za msiba.

Maria 5

Kaka anasema Maria siku zote amekua ni mtu ambaye atakupenda kama unamwambia vitu anavyohitaji kuvisikia lakini kama unamkosoa au kumwambia ukweli atakupotea kama alivyonifanyia mimi, nilimsaidia sana kupata dili la kurekodi na alikua rafiki yangu sana lakini nilipokua naanza kumkosoa hakutaka kuniona tena.

Maria na Morgan

Maria na Morgan miaka kadhaa iliyopita

‘Maria ana miaka hajaonana na ndugu zake wala kuwasiliana nao, kuna kipindi Dada yake huyu (Alison) aliugua sana karibu kufa lakini Maria hakujibu mawasiliano hata tone, sasa hivi anaumwa matatizo ya akili na uti wa mgongo, matibabu anayohitaji wala sio gharama kubwa kwa milionea Maria Carey kushindwa kumuweka dada yake kwenye hospitali nzuri akatibiwa’

Morgan mwenyewe anasema ‘sijaongea na Maria kwa miaka miwili na nusu, nimekua nikisikia taarifa za kulewa kwake kupitia mitandao ya kijamii tu, sidhani hata kama Maria ana mapenzi ya kweli na huyu Mume mtarajiwa wa Australia, naona anaijali ile pete tu… Maria ni mbinafsi, unawezaje kumuacha dada yako anaeumwa kukaribia kufa?’

Maria na mpenzi wake wa sasa ambaye tayari ameshamvisha pete ya uchumba

Maria Carey (45) akiwa na mpenzi wake wa sasa Bilionea raia wa Australia ambaye tayari ameshamvisha pete ya uchumba ambapo harusi hii ikifungwa itakua ni harusi ya tatu kwa Maria Carey.

Dada wa Maria Carey aliwahi kufanya kazi ya kuuza mwili wake miaka ya nyuma kwenye jiji la New York Marekani na anasema ilitokana na kukosa pesa ya kununulia dawa za kulevya na kuihudumia familia yake kipindi hicho Maria Carey hajawa mwimbaji maarufu wa dunia.

Maria 8

Dada wa Maria, Alison alipata ujauzito wake wa kwanza akiwa na umri wa miaka 15, ni mama wa watoto wanne ambapo hajawahi kuongea na Maria Carey toka kulipotokea ugomvi kati yao mwaka 1994, yaani miaka 22 iliyopita.

Maria 7

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

TAARIFA YA AJALI YA BASI ILIYOUA DAKIKA 15 KABLA YA KUSHUSHA ABIRIA UBUNGO DAR ES SALAAM? TAZAMA HII VIDEO HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments