Mix

Maamuzi ya Rais Uhuru Kenyatta kupunguza mshahara wake na wa mawaziri.

on

Screen Shot 2014-03-08 at 12.16.25 PMTaarifa ikufikie kwamba Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametangaza kupunguza mshahara wake na wa Makamu wake William Ruto kwa asilimia 20 na mshahara wa Mawaziri utapunguzwa kwa asilimia 10.

President mwenyewe amesema hii ishu nzima iliafikiwa kwenye mkutano na baraza la Mawaziri uliofanywa kwa siri ambapo amekaririwa akisema ‘tukizingatia hali ya kupanda kwa garama mimi na makamu wangu tunachukua hatua ya kupunguza mshahara wetu, makatibu wakuu wa serikali na makatibu wasaidizi nao wamekubali asilimia kumi kukatwa kwenye mishahara yao kuanzia sasa’

‘Kingine ni kwamba tutaandaa mkataba mpya wa kusafiri ambao utafuta safari za nje ya nchi isipokua zitabaki zile zenye umuhimu tu, serikali yangu inampango wa kupunguza matumizi yanayojirudia na ambayo hayaongezi umaana wowote kwenye ufanyaji kazi’

Tupia Comments