NI Mkali kutokea Bongo Flevani, Marioo ambae Desemba 2 2022 kwa mara ya kwanza atazindua album yake mpya aliyoipa jina la The Kid you Know.
Staa huyo ataizindua kwa mara kwa kwanza album hiyo katika chimbo jipya liitwalo 1245 lilipo Masaki Dar es Salaam.
Album hiyo ina nyimbo zisizopungua 17 akiwa amewashirikisha mastaa mbalimbali akiwemo Dunnie, Alikiba, Jovial, Jux, Loui, Fameica, Rayvanny na wengineo.
Kwa mara ya kwanza Marioo atawasikilizisha wadau mbalimbali wa muziki na mastaa katika kuisikiliza album hiyo usiku wa leo Desemba 2, 2022 katika chimbo liitwalo 1245 lilipo Masaki Dar es Salaam.