Dar es Salaam, Novemba 30, 2022: Jukwaa la kwanza kuwahi kutokea Tanzania la Uwekezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) limefanyika leo Jijini Dar es Salaam na limeratibiwa na UNDP na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwa ushirikiano na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara (MIIT) na Mfuko wa Maendeleo ya Mitaji wa Umoja wa Mataifa (UNCDF).
Mgeni Rasmi alikuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa na dhamira ya jukwaa ni “Wekeza Katika Tanzania Ijayo”.
Jukwaa la Uwekezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu Tanzania linalenga dhumuni la kuzindua Ramani ya Mwekezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu Tanzania na kurahisisha mabadilishano ya mawazo kati ya wawekezaji na shughuli/miradi ambayo inaangukia katika maeneo ya fursa za uwekezaji (IOAs).
Jukwaa linalenga kuweka njia ya mabadilishano ya mawazo kuhusu sera ya taifa ya ajenda ya Tanzania kuhamasisha uwekezaji wa malengo ya maendeleo endelevu na kurahisisha maendeleo nchini.
UNDP, MIIT na TIC wameshirikiana kutengeneza ramani ya mwekezaji wa malengo ya maendeleo endelevu Tanzania, chombo cha taarifa za masoko kinacholenga kuwasaidia wawekezaji katika kufanya uamuzi kwa kubainisha fursa za uwekezaji na aina za biashara kwa kuendeleza malengo ya maendeleo endelevu na mafanikio ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo ya Taifa wa Miaka Mitano (FYDP III).
Kwa njia ya utafiti wa kina na mchakato elekezi uliowashirikisha wadau wa sekta ya umma na binafsi Tanzania pamoja na warsha za uhalali na uendeshaji Dar es Salaam na Zanzibar zinazolenga kupitia matokeo ya ramani ya mwekezaji wa malengo ya maendeleo endelevu Tanzania na kuweka habari za masoko, ramani hiyo ya mwekezaji wa malengo ya maendeleo endelevu Tanzania imeanzisha maeneo 13 ya fursa za uwekezaji (IOAs) pamoja na mifano ya biashara yenye tija na takwimu zinazojitosheleza, ambazo zinaweza kuwaongoza wawekezaji na shughuli za bishara kufanya maisha ya watu Tanzania na duniani kuwa tofauti.
Maeneo ya fursa za uwekezaji yako katika sekta tano za vipaumbele, ambapo mahitaji ya maendeleo ya taifa na vipaumbele vya sera za nchi vinalingana kwa mambo mengine, kama vile chakula na kilimo, rasilimali zinazoweza kurejeshwa na nishati mbadala, miundombinu, elimu na huduma. Nyingi za sekta hizi zinatoa fursa kwa muungano wa kikanda kwa njia ya fursa za minyororo ya thamani inayojitokeza kwenye uamuzi wa biashara unaoweza kufanywa katika Eneo la Biashara Huria katika Bara la Africa (AfCFTA).
Taarifa pana za masoko kutoka Tanzania zinapatikana kwa umma kwenye jukwaa la mwekezaji wa malengo ya maendeleo endelevu kimataifa kupitia HAPA
Jukwaa lilikuwa ni pamoja na kikao cha kipekee kutoka kwa washindi wa mipango ya ukuaji na miradi ya TIC, ambayo inaendana na ramani ya mwekezaji wa malengo ya maendeleo endelevu Tanzania na maeneo ya fursa za uwekezaji kwa wawekezaji.
Aidha, lilihusisha majadiliano ya kuvutia na wadau muhimu kwenye mandhari ya uwekezaji Tanzania na matokeo ya ramani ya mwekezaji wa malengo ya maendeleo endelevu Tanzania vilienda sambamba na kikao cha kipekee cha miradi ya TIC inayoendena na ramani ya mwekezaji wa malengo ya maendeleo endelevu Tanzania na maeneo ya fursa ya uwekezaji yaliyobainishwa na kutolewa kwa wawekezaji watarajiwa.
Lengo la jukwwa ni kurahisha majadiliano ya mawazo kati ya watoaji wa mitaji wa ndani na wa kimataifa chini ya mfumo wa SDGs, mahusiano thabiti ya uwekezaji, washiriki katika biashara, na vyombo baina ya wawekezaji na wafanyabiashara wanaowezesha uelewa wa taarifa za masoko za UNDP na uanzishaji wa mahusiano mapya ya uwekezaji na kuwezesha mitaji mikubwa zaidi ili kurahisisha maendeleo ya malengo ya maendeleo endelevu Tanzania.
Wakati wa kufanyika kwa jukwaa, miradi mitano ya ukuaji wenye tija ya UNDP (GSIV) ilipata fursa kuonyesha bidhaa zake kwa wawekezaji watarajiwa. Mpango wa GSIV ni wa mchakato wa ushindani sana uliozinduliwa na UNDP Tanzania kwa kuanisha shughuli za biashara zenye tija, ulioonyesha masoko bora ya bidhaa, na mfano endelevu wa kipato au ambao unaonyesha tayari uwepo wa uwekezaji. Zaidi ya miradi 80 ilipendekezwa kushiriki kwenye mchakato wa uchaguzi na wawezeshaji, ofisi za kifamilia, mifuko yenye tija, mashirika ya kimataifa na serikali.
“Mpango wa sasa wa Msaada wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDAP II) uko kwenye malengo ya maendeleo endelevu (SDGs), ukilenga jamii zilizo kwenye hatari zaidi. Wakifanya kazi kwa ushirikiano wa karibu, Ofisi ya Umoja wa Mataifa na Serikali ya Tanzania, kwa pamoja wanaendeleza na kutekeleza mipango, sera na njia mpya za kufikia watu wa pembezoni. Lengo la pamoja ni kuhakikisha mgawanyo sawa wa kupata maendeleo kwa makundi ya watu na mikoa na kuchangia kuelekea upatikanaji wa malengo muhimu ya maendeleo endelevu ambayo yataleta matokeo chanya ya watu wa Tanzania,”- alisema Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Aidha, Mwakilishi Mkazi wa UNDP Christine Musisi alieza jinsi UNDP inavyotaka kusaidia na kushirikiana na Serikali katika kurahisisha uwekezaji Tanzania, katika kufikia malengo ya kitaifa na kimataifa kupitia ramani ya mwekezaji wa malengo ya maendeleo endelevu Tanzania.
“Uzinduzi wa ramani ya mwekezaji wa malengo ya maendeleo endelevu unaweza kusanifisha ushiriki wa sekta binafsi katika kusaidia uwekezaji endelevu Tanzania. Hata hivyo, maendeleo ya njia hii yatategemea mahusiano imara kati ya serikali, sekta binafsi na sekta ya fedha na masoko ya mitaji pamoja na UN”- alisema Dk Ashatu Kijaji, Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara.