Asha Nkunti mkazi wa jijini Dodoma ambaye amekatwa titi lake moja baada ya kuugua maradhi ya Saratani.
Asha anasema mwaka 2009 aligundulika kua na Saratani ya titi na kupelekea kukatwa titi lake.
Anasema haikuwa kazi rahisi kupokea majibu ya vipimo na kutakiwa kukatwa titi kwani aliamini kuwa ndio utakuwa mwisho wa maisha yake kwani watu wengi husema ugonjwa huo hauna dawa .
Hivyo baada ya kushauriwa na madaktari alikubali kufanya Operesheni lakin kwa Sasa amepona na ameweka titi la bandia na bila watu kujua hivyo kuwahi matibabu mapema anasema kumemsaidia kupona haraka na kuendelea na shughuli zake
Kutokana na changamoto hiyo ikamlazimu Kaimu Mganga Mkuu Manispaa ya Morogoro Daktari Felista Stanslaus kutoka wito Kwa jamii kua na utaraibu wa kupima afya Mara kwa Mara hasa magonjwa ya Saratani.
Amesema kutofanya vipimo vya awali vya kitabibu, hupelekea walio wengi kubainika katika hatua za mwisho za ugonjwa huo Jambo ambalo ni changamoto kwenye kupata Matibabu.
Kukosekana kwa Uhasishaji wa Watu kujitokeza kupima afya zao, ndiko kumeisukuma Taasisi ya Saratani ya Matiti Tanzania kufika Morogoro kutoa elimu, ushauri na namna ya kutambua umhimu wa kufanya vipimo hivyo.
Sharon Kuzilwa ni Mkurigenzi kutoka Taasisi ya hiyo anasema wanatarajia kuwafikia watu zaidi ya elfu moja huku msukumo wake ni kujikita vijijini .