Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Daniel Chongolo ametoa siku kumi na nne kwa waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Angela Kairuki kufika katika kituo cha afya Mikese kilichopo Wilayani Morogoro baada ya majengo ya huduma ya mama na mtoto yaliyopo katika kituo hicho kutelekezwa kwa zaidi ya miaka mitatu.
Katibu Mkuu Daniel Chongolo amesema hayo mara baada ya kuwasili katika kituo hicho cha afya katika muendelezo wa siku ya pili ya ziara yake Wilayani Morogoro na kusisitiza haiwezekani kuona Serikali ya Chama cha Mapinduzi kuwekeza zaidi ya shilingi milioni 400 katika ujenzi wa miundombinu hiyo ya afya lakini bado hakuna tija kwa wananchi.
Baadhi ya wananchi wamesema kukamilika kwa kituo hicho cha afya kutawasaidia kuwapunguzia adha wakina mama wajawazito kutembea umbali mrefu kufuata huduma za mama na mtoto nje ya eneo hilo la Mikese.
KATIBU MKUU CCM AMTAKA WAZIRI TAMISEM SIKU 14 AFIKE MIKESE HOSPITALI,AGUNDUA MADUDU UJENZI WAKE