Ommy Dimpoz amerudi Tanzania March 10 2014 saa tano usiku ambapo AyoTV na millardayo.com ziliweza kumnasa baada ya kushuka.
Amethibitisha ni kweli amefanya video yake mpya London ambapo aliehusika kama Director ni mshkaji ambae amefanya video kadhaa za wakubwa wa Afrika kama Azonto ya FUSE ODG, video za caro ya Wizkid na Davido ‘skelewu’
Hizi zinazofata hapa chini ni baadhi ya pichaz tu za utengenezwaji wa video hii mpya ya Ommy Dimpoz huko London.
Huyu hapa chini ndio Director mwenyewe anaitwa Moe Musa Mwingereza mwenye asili ya Nigeria ambae unaambiwa gharama ya video anazozifanya ni kuanzia dola za kimarekani elfu 20 na kuendelea, kwa haraka haraka ni zaidi ya milioni 30.
Hizi hapa chini ni baadhi ya picha za Ommy Dimpoz akiwasili Airport Dar es salaam usiku wa March 10 2014.