AyoTV

Baada ya Tunda man kuzawadiwa benz na shabiki, huyu ni msanii mwingine bongo aliezawadiwa hili gari

on

Screen Shot 2014-03-12 at 1.51.39 PMKwenye moja kati ya Exclusive za millardayo.com mwaka juzi kabla ya AyoTV kuanza kufanya kazi online, ilikua ile stori ya msanii Tunda Man ambae alionyesha gari aina ya Benz alilozawadiwa na shabiki yake wakati alipokwenda kufanya show Uingereza ambapo alifanikiwa kuileta hiyo Benz bongo.

Leo hii kwenye Exclusive ya AyoTV, msanii Alawi Juniour ambae ameshawahi kufanya kazi kwenye band ya T.I.D amekua msanii mwingine kukiri kuzawadiwa gari na shabiki wake ambae ilitokea tu alikua anamuonaona mtaani.

Alawi anasema kabla ya hapa hakuwahi kumiliki gari na wala hiyo haikua ishu kubwa sana kwake ila kafurahia hii zawadi ambayo hakuitarajia kutoka kwa huyu fan ambae anayo magari mengi tu ndio maana akampa hili ambalo pia alitoka nalo Uingereza.

Ukihitaji kuliona vizuri na kujua info nyingine unaweza kutazama hii video hapa chini mtu wangu na utakua umeisupport AyoTV.

Ili kuwa karibu zaidi na kila stori inayotokea, karibu ujiunge na mimi kwenye twitter, facebook na instagram kwa jina hilohilo la Millard Ayo.

)
Video yake mpya ya ‘Love matata’ ft Rich Mavoco ndio hii hapa chini

)

Tupia Comments