Habari za Mastaa

J.lo angekuta Diddy na Ben Affleck wanaelea kwenye maji angemuokoa nani kati yao?

on

Screen Shot 2014-03-15 at 12.50.51 PMMwimbaji Jennifer Lopez ameshawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mastaa kadhaa wa dunia akiwemo Diddy, Ben Affleck na baadae akaolewa na Marc Anthony.

Kwenye interview aliyofanyiwa hivi karibuni, aliulizwa kama ingetokea yuko kwenye boti baharini alafu akawaona Ben Affleck na Diddy wanaelea kwenye maji na wanahitaji msaada, huku J.Lo akiwa na nafasi ya kumuokoa mmoja tu kati ya hawa angemuokoa nani?

Screen Shot 2014-03-15 at 12.54.19 PMKwa utani J.lo alijibu akiwa anacheka na kusema angewaacha wote wafie mbele ila sekunde chache baadae akasema alikua anatania na kwamba kutoka moyoni mwake anawapenda wote na hata wao wanajua anawapenda.

Unaweza kutazama jinsi ilivyokua kwenye hii video hapa chini…

Tupia Comments